Chelsea inaweza kumruhusu winga wake, Pedro Rodriguez kuondoka klabuni hapo haswa kutokana na umri wake na uwezo kuonekana kushuka uku kukosa kuanza kwenye kikosi cha kwanza kukitajwa kama sababu kubwa.
Willian pia anahusishwa kutakiwa kwa karibu na klabu ya Barcelona uku mkataba wake klabuni Chelsea ukimalizika mwishoni mwa msimu huu.
Chelsea inahusishwa kwa karibu kumtaka winga wake wa zamani ambaye baadae alijiunga na Sassuolo jumla kwa usajili unaotajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 3, Jeremie Boga.
Mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo, Giovanni Carnivelli amejitokeza na kuweka wazi juu ya fununu na taarifa hizo za Chelsea kumtaka winga huyo ambapo amesema "Tumekuwa na mazungumzo na Chelsea toka kipindi cha sikukuu za Christmass mwaka jana."
"Tupo tayari kumuachia nyota huyo ajiunge tena na Chelsea kwasababu sisi wawili tuna uhusiano mzuri sana. Tuna ukaribu mzuri."
"Kama Chelsea ipo tayari kumsajili nasi tupo tayari ili tuendelee kuzidisha ukaribu wetu na wao."
Inaelezwa nyota huyo anapatikana kwa paundi milioni 12.
No comments:
Post a Comment