Hapa nakuletea baadhi ya mambo machache aliyoyazungumza kwenye mahojiano hayo;
"Kwa upande wangu mpaka sasa umekuwa ni msimu mzuri kwangu. Haswa utamu unazidi maana kuna michezo mingi mizuri na mikubwa bado inakuja."
"Kuichezea klabu kama Chelsea mara zote kunaleta presha. Kwa upande wangu natakiwa kuwa mahali sahihi kwa muda sahihi, na kujiamini mwenyewe na kuuamini uwezo wangu. Naamini bado kuna magoli machache naweza kuyafunga. Napenda kucheza mahali penye presha."
"Kama timu huwa kuna vipindi vya kupanda juu na kushuka, ulikuwa wakati mgumu tulipofika kipindi hiko cha kushuka. Tulipoteza michezo kadhaa lakini sasa tunajaribu kujiweka sawa."
Akizungumzia kipindi cha mapumziko ambacho wachezaji wamekipata, amesema "Hiki kipindi cha mapumziko ni kipindi muhimu kwetu maana kuna michezo mikubwa inakuja na tunatakiwa kuwa sawa kimwili na kujiandaa vyema."
No comments:
Post a Comment