Familia na marafiki wa nyota huyo wameeleza kipa huyo alipoachana na mpenzi wake wa zamani, Andrea Perez ambaye walianza mahusiano toka utotoni ndiyo sababu ya kipa huyo kushuka kiwango na kutishia nafasi yake kikosini Chelsea na kwenye kikosi cha taifa cha Hispania kitakachocheza michuano ya Euro miezi kadhaa ijayo.
Kupitia gazeti la nchini Hispania, Mundo Deportivo, inaelezwa mlinda mlango huyo amekuwa hayupo kwenye kiwango kizuri kutokana na upweke huo na ushahidi mmojawapo ni kutokana na picha alizokuwa anazituma kwenye mtandao wa Instagram.
Kuna picha aliyoituma akiwa mapumzikoni ufukweni mwaka 2018 akiwa mapumzikoni na mpenzi wake huyo uku wakionekana wakiwa na furaha.
No comments:
Post a Comment