Fabregas atua nchini Urusi - Darajani 1905

Fabregas atua nchini Urusi

Share This

Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas hajafanikiwa kuchaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambacho kinashiriki michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko nchini Urusi.

Jioni hii timu yake hiyo inacheza mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambapo inamenyana dhidi ya Urusi ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo, licha ya kutokuitwa kwenye timu yake bado haijawa sababu ya kufika nchini humo ili kuwa moja ya mashabiki wa kuipa nguvu timu yake.

Kupitia mtandao wa Instagram, nyota huyo ametuma ujumbe wa picha akionekana yupo nchini Urusi na bila shaka atakuwepo uwanjani akiutazama mchezo huo akiwa kama shabiki lakini nahodha wake msaidizi klabuni Chelsea, Cesar Azpilicueta akiwa moja ya wachezaji kwenye kikosi hicho.

Kupata habari za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡Darajani1905

No comments:

Post a Comment