Nyota wa zamani wa Chelsea, John Obi Mikel ambaye ameiongoza timu yake ya taifa ya Nigeria kwenye michuano ya Kombe la Dunia ambapo imeshindwa kuvuka hatua ya makundi amefunguka kiundani kwamba ni sababu gani haswa iliyomfanya akakataa kutua Man utd na kuamua kutua Chelsea hiyo ikiwa ni mwaka 2005.
Nyota huyo anasimulia kwamba baba yake alitaka atue Man utd ambayo ilikuwa ikifundishwa na kocha ambaye baba yake alikuwa akimhusudu, Sir. Alex Fabregas na hata watu wake wa karibu walipendekeza atue klabuni huko.
Lakini wakati akifanya mawasiliano na kocha huyo, huku mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich akamfata kijasusi kwa kumchukua na kumweka kisiri kwenye hoteli ambayo hakuna mtu aliyejua Mikel yupo wapi lakini mwisho wa siku kwa kuwa alikuwa mdogo kiumri (alikuwa na miaka 18) ilikuwa ikimchanganya kuamua wapi ahamie.
Ila kutokana na alitoka kufanya vyema na kikosi cha Nigeria kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana kwa mwaka 2005 huku akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa pili wa michuano hiyo aliambatana na wachezaji wenzake wa Nigeria ambao alikuwa akiishi nao hotelini hapo alipohifadhiwa na Abramovich.
Na kama angeamua kuachana na Chelsea basi ingemaanisha wenzake hao wasingepata nafasi ya kufanya majalibio kwenye klabu za soka maana wangekosa pakuishi na hivyo kwa kuwa nyota huyo alihitaji kuwa na watu wa karibu akaamua kuchagua kutua Chelsea ingawa mwenyewe anakiri kwamba ulikuwa ni uamuzi mgumu kwake haswa kutokana na nafasi ya kiungo kuwa na nyota waliokuwa bora kipindi iko. Frank Lampard, Michael Ballack na Makelele. Lakini pia haachi kukiri kwamba hajutii kutua Chelsea mahali ambapo ameshinda nayo mataji kibao likiwamo la klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2012 kabla ya kuondoka mwaka 2017.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡Darajani 1905
No comments:
Post a Comment