Uchambuzi; Kuelekea mchezo wa Huddersfield vs Chelsea (11-Agosti-2018) - Darajani 1905

Uchambuzi; Kuelekea mchezo wa Huddersfield vs Chelsea (11-Agosti-2018)

Share This

Tarehe 11-Agosti mwaka huu 2018 kutachezwa mchezo wa kwanza kwa Chelsea katika michuano ya ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2018-2019 ambapo itakuwa ugenini ikimenyana dhidi ya Huddersfield.

Mchezo huo pia utachezwa siku sita mara baada ya kikosi cha Chelsea kucheza mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ambapo itamenyana dhidi ya Manchester city katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Manchester city atakuwa akicheza kama bingwa wa ligi kuu kwa msimu ulioisha wakati Chelsea atacheza akiwa kama bingwa wa Kombe la FA. Mchezo huo utachezwa tarehe 5-Agosti.

Chelsea ina historia ndefu dhidi ya Huddersfield ambapo mara ya kwanza kabisa kwa klabu hizo kukutana ilikuwa mwaka 1911 ambapo Chelsea iliondoka na ushindi wa magoli 2-0 na mchezo wa mwisho uliochezwa mwaka huu katika mzunguko wa pili wa ligi kuu msimu uliopita.

Lakini je wajua kwamba toka mwaka 1964 wakati Tanganyika ilipoungana na Zanzibar ili kuiunda nchi ya Tanzania, Chelsea imepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Huddersfield? tena mchezo huo ulikuwa wa kombe la ligi. Toka mwaka huo Chelsea imeshinda michezo 10 na kupoteza mchezo mmoja.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment