Moja kati ya mazao ambayo Chelsea inasifika kwa kuwakuza ni kiungo raia wa Uingereza, Ruben Loftus-Cheek ambaye kwa sasa anaitumikia timu yake ya taifa kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Cheek mwenye miaka 22 ameichezea Chelsea michezo 32 tu toka alipopewa nafasi ya kwanza ya kuichezea klabu hiyo mchezo wa kwanza mwaka 2014 na msimu uliopita aliutumia akiwa kwa mkopo kwenye klabu ya Crystal Palace ambapo huko alitamba na kufanya vyema kabla ya kupata majeraha yaliyomweka nje kwa muda mrefu.
Nyota huyo amehojiwa na kuulizwa anadhani kwanini maisha ya nyota makinda wanaochipukia kutoka kwenye akademi yanakuwa magumu.
Nyota huyo alijibu kwa kusema klabuni hapo kumekuwa na ugumu kwa wachezaji makinda kupata nafasi huku vijana hao wakifanikiwa kufanya mazoezi na mastaa wa kikosi cha kwanza lakini hakuna nafasi wanayopewa haswa kwake yeye ambaye anaamini soka lake lilikuwa bora kwa muda mrefu lakini kutokana na kutopewa nafasi ikawa ngumu kujiweka sawa.
Cheek alipoulizwa anadhani kipi hakiendi sawa klabuni Chelsea kuhusu vijana kukosa nafasi, nyota huyo alisema "Kuna makocha ambao wanapenda kuwapa nafasi vijana, makocha kama Southgate (kocha mkuu wa Uingereza) pamoja na Roy Hodgson (wa Crystal Palace) lakini ni tofauti na Antonio Conte. Nadhani presha ya kutaka matokeo ndo inamfanya kuogopa kuwatumia vijana" alisema nyota huyo.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment