Nyota wa Chelsea, Cesar Azpilicueta pamoja na mwenzake Andreas Christensen walikuwa na majukumu makubwa kwenye timu zao za taifa katika michuano ya Kombe la Dunia huko nchini Urusi.
Azpilicueta alikuwa moja ya wachezaji wa kikosi cha timu yake ya taifa ya Hispania ambao walikuwa wanacheza mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Urusi lakini bahati haikuwa kwao wakapoteza kwenye penati mara baada ya muda wa kawaida na dakika 30 za nyongeza kuisha kwa sare ya 1-1. Azpilicueta hakupata nafasi ya kujumuishwa na badala yake akawa kama mchezaji wa akiba.
Christensen alikuwa akiiongoza timu yake ya taifa ya Denmark kucheza dhidi ya Croatia na huko nako mambo hajawa vizuri mara baada ya muda wa kawaida ukiongeza na dakika 30 za nyongeza kuisha kwa sare ya 1-1 na walipofika kwenye matuta wakatolewa kwa penati 3-2.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment