Naamini tukio ili lilionwa na watu wachache sana lakini kwa kuwa sitaki nkukoseshe uhondo huu.
Bila shaka nkikuuliza wachezaji wanaotamba kwa vituko basi utantajia jina la David Luiz ambaye ni kipenzi cha watoto lakini naamini utantajia jina la Rudiger ambaye siku za mwishoni mwishoni mwa msimu amekuwa akicheza sana kwa vituko. Najua ukivuka sanaaa utamtaja Eden Hazard.
Nina uhakika kabisa hutokuwa na wazo la kumtaja nahodha msaidizi wa Chelsea, Cesar Azpilicueta. Amekuwa haonekani kuwa na vituko sanaa, ukimuona uwanjani muda wote ni mtu wa kazikazi huku akichomekea fulana yake.
Sasa kuna tukio moja alilifanya lilibaki kuwa kituko cha mwaka, unajua ni tukio gani?
Ilikuwa kwenye mchezo wa kirafiki ambapo Chelsea ilikuwa ikicheza dhidi ya Thailand All-stars huko Bangkok mwaka 2015. Mchezo huo ulichezwa mara baada ya Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2014-2015 kwa hiyo walikuwa wanacheza mchezo huo kama mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu wa 2015-2016.
Basi mchezo huo ukachezwa na Chelsea ikashinda kwa goli 1-0 lililofungwa na kinda wa Chelsea wakipindi iko, Dominic Solanke ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Liverpool. Sasa kituko kilitokea mara baada ya mchezo kumalizika ambapo mwamuzi wa mchezo huo alimfata Hazard na kuomba kupiga nae picha (selfie), tukio hilo la mwamuzi likamfanya Azpilicueta kumfata mwamuzi na kumchukulia kadi ya njano na kumpa mwamuzi kwa kosa la kuomba kupiga picha na Hazard.
Tukio hilo lilimfanya kila mtu kubaki na kicheko tu..
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment