Chelsea na klabu nyengine za bara la Ulaya zipo vitani zikigombania saini ya kiungo raia wa Urusi, Aleksander Golovin huku kukiwa na taarifa zinazodai kwamba Chelsea ipo kwenye mazungumzo ya kumnasa nyota huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri akiwa na timu yake ya taifa huko kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Golovin ambaye anaichezea klabu ya CSKA Moscow ya nchini Urusi anatajwa kufukuziwa na Chelsea inayoripotiwa kuwa tayari kutoa paundi milioni 27 ili kumnasa kiungo huyo
Mama mzazi wa kijana huyo mwenye miaka 22 amefanyiwa mahojiano na kuulizwa lipi analifikiria kuhusu mwanae huyo ambaye kwa sasa ni lulu sokoni, na mama yake amesema nyota huyo ana nafasi ya kufanya maamuzi yoyote lakini anahitaji nafasi zaidi ya kuweza kumaliza majukumu aliyokuwa nayo kwa sasa akiwa na timu yake ya taifa na kisha ataamua mara baada ya michuano hiyo kumalizika.
Chelsea inaweza kuwa na nafasi kubwa ya kumnasa haswa kutokana na klabu ya kiungo huyo, CSKA Moscow inamilikiwa pia na mmiliki anayeimiliki Chelsea, Roman Abramovich.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment