Kombe la Dunia; Willian uso kwa uso na Hazard? - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Willian uso kwa uso na Hazard?

Share This

Kama ilivyoada, kama ilivyo kawaida, jioni ya leo kunachezeka tena michezo ya Kombe la Dunia kwa hatua ya 16 bora huku nyota wa Chelsea wakihusika kuzisaidia timu zao kucheza michezo ya leo.

Willian Borges da Silva ndo atakuwa nyota wa kwanza wa Chelsea kushuka uwanjani jioni ya leo ambapo ataiongoza timu yake ya taifa ya Brazil kucheza dhidi ya ndugu zao wa bara la Amerika ya Kusini, Mexico.

Willian anaweza akatumika kwenye mchezo huu kama chaguo la kwanza na kama akifanikiwa kuiongoza kupata ushindi basi atamsubiri mshindi wa mchezo mwengine wa hii leo utakaochezwa saa 21:00 kwa saa za Afrika Mashariki ambao unawakutanisha Ubelgiji yenye nyota wenzake wa Chelsea itakayocheza dhidi ya Japan.

Ubelgiji yenye nyota wa Chelsea Eden Hazard, Michy Batshuayi na Thibaut Courtois watapambana kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wao wa usiku wa leo wakishuka uwanjani kumenyana dhidi ya Japan.

Kama Hazard akiisaidia Ubelgiji kupata ushindi basi anaweza akakutana na rafiki yake klabuni Chelsea, Willian

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment