Chelsea yamtumia Willian kuitega Barcelona - Darajani 1905

Chelsea yamtumia Willian kuitega Barcelona

Share This

Siku kadhaa zilizopita kulisambaa taarifa kwamba klabu ya nchini Hispania inayoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama La Liga, Barcelona inamfukuzia nyota wa klabu ya Chelsea, Willian Borges da Silva.

Taarifa hizo zilidai kwamba Barcelona iliandaa paundi milioni 50 ili kumnasa Willian lakini Chelsea ilikataa kupokea fungu hilo.

Sasa tena hii leo kumetoka taarifa mpya ikidai klabu ya Chelsea imetaja fungu inalotaka ili kumuuza nyota huyo raia wa Brazil. Paundi milioni 70 imetajwa na klabu hiyo kuwa ndio dau ambalo linaweza kumng'oa nyota huyo kuondoka klabuni hapo.

Lakini pia taarifa hizo zinazidi kusema kwamba Barcelona imegoma kutoa dau hilo haswa kutokana na umri wa Willian wakidai kutoa paundi milioni 70 kwa mchezaji mwenye miaka 30 ni biashara ambayo haina maana.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment