Chelsea yavunja rekodi tuzo za Ballon d'Or - Darajani 1905

Chelsea yavunja rekodi tuzo za Ballon d'Or

Share This

​Hii leo kumefanyika shughuli ya kutaja wachezaji ambao wanawania tuzo za Ballon d'Or zinazotolewa na shirika la utangazaji nchini Ufaransa.


Wachezaji wa Chelsea nao walikuwa sehemu ya orodha hizo ambapo wachezaji wa Chelsea ya wanaume wameweka rekodi ya kutoa wachezaji watano na kuifanya Chelsea kufungana na Man city kwenye orodha ya klabu za soka la wanaume kwa kutoa idadi kubwa.


Wachezaji hao ni N'Golo Kante, Jorginho Frello, Cesar Azpilicueta, Romelu Lukaku na Mason Mount ambaye yeye anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka kwenye akademi ya Chelsea kuwania tuzo hiyo toka John Terry alipofanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 2005.


Lakini pia Edoaurd Mendy yeye anawania tuzo ya kipa bora maarufu kama Trophee Yachine ambayo pia anagombania na vigogo wengine.


No comments:

Post a Comment