Aliyewai kuwa mchezaji wa Chelsea ambaye ni raia wa nchini Liberia barani Afrika, George Weah ameshinda uchaguzi mkuu wa nchini Liberia ambapo alikuwa anagombania nafasi ya urais wa nchi hiyo.
Gorge Weah ameshinda nafasi hiyo kwa kuchaguliwa katika majimbo (Counties) yapatayo 12 kati ya 15 ya nchini Liberia huku mshindani mwenzake au mpinzani wake Joseph Boakai akipata majimbo mawili tu. Kupitia mtandao wa Twitter, George Weah ametuma ujumbe kuwashukuru raia wa Liberia kwa nafasi hiyo waliompatia akishukuru pia kwa kuaminika na wananchi wa nchi yake.
George Weah aliwai kuichezea Chelsea kwa mkopo akitokea AC Milan ambapo hakukaa sana klabuni hapo akicheza michezo 15 tu huku akifunga magoli 5.
"Ni jambo lenye hisia kali napenda kuwashukuru raia wote wa Liberia kwa kunipatia kura zenu. Ni alama ya tumanini kubwa sana kwangu" alituma maneno hayo katika mtandao wa Twitter.
George Weah pia anakumbukwa vizuri kwa kuwa mwafrika wa kwnza kutwaatunzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d'or pamoja na kushinda tunzo ya mchezaji bora wa mwaka iliyotolewa na FIFA ambapo hiyo ilikuwa miaka ya 1995. Aliwai pia kuzichezea klabu za AC Milan pamoja na Mama site (Manchester city).

NYOTA WA CHELSEA AWA RAIS LIBERIA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment