WENGER AMKOSOA MOURINHO - Darajani 1905

WENGER AMKOSOA MOURINHO

Share This
Kocha wa klabu ya Asenyani (Arsenal), Arsene Wenger amemcheka kocha mwenzake wa Manyumbu (Manchester united), Jose Mourinho ambaye kabla alishawai kuifundisha Chelsea.

Kocha Wenger amemcheka kcha huyo mara baada ya kusikia maneno ya kocha huyo akisema klabu yake ya Manyumbu haifanyi vizuri kutokana na kutotumia kiasi kikubwa kwenye usajili kabla ilivyofanya kklabu ya Mama site (Manchester city) inayoongoza ligi kuu Uingereza kwa sasa.

"Sidhani kama ni sahihi kama kocha kulalamika eti kwaanini mpinzani wangu anasajili kwa kiasi kikubwa ni kupambana kama mi navyopamban" alisema kocha huyo raia wa Ufaransa ambaye amekuwa akiingia kattika migogoro mara kadhaa na kocha mwenzake huyo.

"Yani ni kama eti leo nina miaka 21 kwenye klabu alafu nije hadharani na kusema sipendezwi na klabu flani inavyosajili, sidhani kama ntakuwa sahihi. Kuna klabu kubwa hapa Uingereza ammbazo zina hela kuliko Arsenal ila siwezi kusema leo kuwa sipendezwi na klabu fulani maana nimekuwa hapa kwaa miaka 21 na mambo hayo hayajaanza leo" alisema Wenger.

Kocha Jose MOurinho alilalamika jana mara baada ya mchezo dhidi ya Burnley ambapo klabu yake iitoka suluhu ya 2-2 na kuilaalamikia klabu yake kuwa haijafanya vizuri kutokana na kutotumia kiasi kikubwa kwenye usajili kama ilivyofanya Mama site.

Takwimu zikionyesha jinsi Jose Mourinho (Man utd) na Pep Guardiola (Man city) kiasi walichotumia sokoni kununua wachezaji

No comments:

Post a Comment