MANENO YA MESSI YAIFANYA MADRID IACHANE NA HAZARD - Darajani 1905

MANENO YA MESSI YAIFANYA MADRID IACHANE NA HAZARD

Share This
Yani kama upo karibu na mama ntilie mwambie akupe chochote unachotaka mwambie mi ntakuja kulipa, hahaaaaaa! we usichukue mi nakutania tu, yote hii ni furaha, tumetoka kupata habari mbaya ya Kante kutakiwa na Real Madrid lakini sasa tumepata habari nzuri inayoweza kutufanya tufurahi na kushinda wiki nzima tunacheka mara baada ya kupata taarifa hii.

Unajua imekuwaje? Kwa taarifa zilizopo ni kuwa, tajiri na mmiliki wa klabu ya Real Madrid, Fiorentino Perez amesitisha mpango wake wa kumsajili nyota wa Chelsea, Eden Michael Hazard.


Ndio amesitisha mpango huo wa kumsajili Hazard amara baada ya nyota huyo raia wa Ubelgiji kutoa maneno ya kumsifia nyota wa Barcelona, Lionel Messi ambaye amekuwa na upinzani mkubwa na nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo wakati alipoulizwa kuhusu anauchukuliaje mchezo wa hatua ya 16 bora ambapo ataiongoza Chelsea kumenyana dhidi ya Barcelona.

Eden Hazard alipoulizwa anauchuliaje mchezo huo alisema "Ni jambo zuri na jema kwangu kucheza na klabu bora duniani kama Barcelona na pia kucheza dhidi ya mchezaji bora duniani kwa sasa, Lione Messi" ambapo kwa maneno hayo inaripotiwa ndiyo yamemkasirisha Fiorentino Perez akikasirishwa kwa Hazard kumsifia nyota wa klabu ambayo haipatamani na klabu yake ya Real Madrid na sasa inaelezwa atamtafuta nyota mwengine kama mbadala wa Hazard.

No comments:

Post a Comment