SIMEONE AMPOKEA COSTA, NAYE AIKABIDHI CHELSEA NYOTA HUYU - Darajani 1905

SIMEONE AMPOKEA COSTA, NAYE AIKABIDHI CHELSEA NYOTA HUYU

Share This
Anaitwa Yannick Ferreira Carrasco, winga machachari wa klabu ya Atletico Madrid sasa awekewa njia nyeupe kutua kwa wababe Chelsea mara baada ya kocha wake wa Atletico, Diego Simeone kumruhusu nyota huyo raia wa Ubelgiji aondoke klabuni hapo huku akiushawishi uongozi wa klabu umuuze nyota huyo.

Chelsea ilishawai kutajwa kumuwania Carrasco mwanzoni ingawa dili hilo lilipigwa chini lakini sasa kocha Simeone yupo tayari kumuuza nyota huyo ambaye ameingia katika ugomvi na nyota wenzake klabuni Atletico huku pia akigombana na kocha wa viungo wa klabuni hiyo hali iliyomfanya Simeone kukasirishwa na tabia ya nyota huyo mwrnye miaka 24, na kuamua kumuuza.

Chelsea endapo ikirudisha rada zake za kumuwania Carrasco basi itapata upinzani mkubwa kutoka kwa Bayern Munich na Arsenal ambazo zote zinatajwa kumuwania nyota huyo anayesifika kwa kuwa na kasi na uwezo mkubwa.

Aliyekuwa nyota wa Chelsea, Diego Costa yeye ameungana na klabu yake ya zaman ambayo ni Atletico Madrid ingawa hana ruhusa ya kucheza mpka mwezi ujao kutokana na timu hiyo kuwa na adhabu. Kwa maana hiyo kama dili hili likikamilika itakuwa ni kama vile kumefanyika mabadilishano yaani Diego Costa ameenda Atletico huku Carrasco akija Chelsea.

*Je Chelsea kwa hali hii ya sasa ilivyo ikiwa inaelekea katika nusu msimu mgumu unadhani inamhitaji mtu kama Carrasco au iachane nae?

No comments:

Post a Comment