Chombo cha habari cha nchini Italia, Corriere Dello Sport limeripoti kwamba nyota wa klabu ya Juventus, Danielle Rugani anaweza kutangazwa kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Chelsea katika siku hizi za karibuni.
Taarifa hizo ambazo zimetaarifiwa pia na gazeti la Metro kwamba Chelsea imefikia makubaliano binafsi na mlinzi huyo mwenye miaka 23 huku dau la paundi milioni 35 likitajwa kutumika kwa Chelsea kumnasa nyota huyo.
Rugani ambaye anasifika kwa uwezo wake mkubwa hapati nafasi ya kucheza zaidi kwenye kikosi cha Juventus ambapo kuna wakongwe Chiellini na Benatia.
Kupata habari zote za za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡Darajani 1905
No comments:
Post a Comment