Jana ilikuwa ni siku ya furaha kwa nyota wawili wa Chelsea, N'Golo Kante pamoja na Olivier Giroud ambao waliisaidia timu yao ya taifa ya Ufaransa kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mara baada ya kuitandika Argentina magoli 4-3.
Sasa leo ni zamu ya nyota wengine wawili ambapo Andreas Christensen ambaye ndiye mchezaji bora chipukizi klabuni Chelsea kwa msimu wa 2017-2018 ataiongoza timu yake ya taifa kumenyana dhidi ya Croatia.
Mchezo wa mchezo huo atacheza robo fainali na mshindi wa mchezo mwengine utakaochezwa leo hii kati ya Hispania yenye nyota wa Chelsea, Cesar Azpilicueta Tanco ambao watacheza dhidi ya Urusi ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡Darajani 1905
No comments:
Post a Comment