Kitambo; Abramovich ainunua rasmi Chelsea - Darajani 1905

Kitambo; Abramovich ainunua rasmi Chelsea

Share This

Leo ni tarehe 1-Julai-2018, ni siku mosi katika mwezi wa saba, siku ambayo inamaanisha wachezaji wanaanza mwaka mwengine kwenye mikataba yao. Kama mchezaji alibakiza miaka mitatu kwenye mkataba wake basi mpaka kufikia leo inakuwa imebakiza miaka miwili. Yani tarehe ya leo ndo kama mwaka mpya kwenye mikataba ya wachezaji.

Lakini leo pia ni siku muhimu klabuni Chelsea, ni siku muhimu kwakuwa ni kumbukumbu ya mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kuinunua klabu hiyo miaka 15 iliyopita. Ilikuwa ni mwaka 2003 kipindi iko Chelsea ilikuwa inafundishwa na kocha Claudio Ranieri.

Alitumia dau la paundi milioni 140 kumkabidhi mmiliki wa zamani wa klabu hiyo, Ken Bates ili kuinunua klabu hiyo.

Tajiri huyo raia wa Urusi aliinunua klabu hiyo ambayo kipindi hicho haikuwa na mafanikio makubwa lakini toka amefika yeye klabuni hapo akafanya mapinduzi makubwa akitumia pesa kibao kuijenga timu hiyo akisajili nyota wakubwa ambao mwanzoni ilikuwa ni ngumu kusajiliwa.

Toka ametua klabuni hapo ameisaidia Chelsea kushinda mataji mengi makubwa  klabu bingwa barani Ulaya, ligi ya Ulaya (Europa League), ligi kuu Uingereza, kombe la FA, kombe la ligi, ngao ya hisani na mataji mengine kibao.

No comments:

Post a Comment