Nyota wa Chelsea, N'Golo Kante na Olivier Giroud wameisaidia timu yao ya taifa ya Ufaransa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mara baada ya kuiongoza timu yao kupata ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya Argentina.
Mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Kazan Arena umeshuhudia nyota hao kuiwezesha timu yao kuitupa nje ya mashindano hayo timu ya Argentina ambayo ni ya nyota mwenzao wa Chelsea, Willy Caballero ambaye hakupata fursa ya kucheza mchezo huo.
Sasa Ufaransa inamsubiri mshindi katika mchezo wa baadae kati ya Ureno dhidi ya Uruguay ili kucheza nae katika hatua ya robo fainali.
Hongereni nyota wetu...
No comments:
Post a Comment