Sarri kutangazwa kocha mpya wa Chelsea - Darajani 1905

Sarri kutangazwa kocha mpya wa Chelsea

Share This

Mwanzoni ilikuwa inaripotiwa zaidi na vyombo vya habari vya nchini Italia ambapo anapatikana kocha Maurizio Sarri kwamba Chelsea inakaribia kumnasa kocha huyo. Lakini mara zote hizo hazijakamilika.

Lakini sasa kuonyesha kwamba usajili huo unaenda kukamilika, taarifa za kocha huyo kutua Chelsea zimetolewa na mwandishi maarufu na anayeaminika, Matt Law ambaye ameripoti kwamba Chelsea itamtambulisha kocha huyo wiki ijayo.

Mwandishi huyo ambaye anafanya kazi kwenye gazeti la The Telegraph ameripoti kwamba Chelsea inakaribia kumsainisha kocha huyo aliyetamba na klabu ya Napoli kuanzia wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment