Michezo ya Kombe la Dunia bado inaendelea na kwa sasa ni hatua ya makundi na hapa nakuletea habari kuhusu michezo inayowahusisha nyota wa Chelsea wakiziwakilisha timu zao za taifa kwenye michuano hiyo.
Nigeria 0-2 Croatia
Ni mwanzo mbaya kwa Nigeria ikiwa na nyota wa Chelsea kama Victor Moses pamoja na Kenneth Omeruo ambapo wanashindwa kuanza vyema wakipoteza kwa magoli 0-2 dhidi ya kikosi hicho cha Croatia.
Peru 0-1 Denmark
Nyota wa Chelsea kwenye kikosi cha Denmark, Andreas Christensen wanafanikiwa kuondoka na ushindi katika mchezo wao wa kwanza na kukifanya kikosi hicho cha kinda bora klabuni Chelsea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufudhu.
Brazil vs Switzerland
Willian atashuka uwanjani leo katika mchezo wao wa kwanza ili kumenyana dhidi ya kikosi cha Switzerland. Kuna uwezekano mkubwa kwa Willian kujumuishwa kwenye kikosi cha leo kwenye kikosi cha kwanza cha Brazil.
Ujerumani vs Mexico
Kuna uwezekano kwa Antonio Rudiger naye kuteuliwa kwenye kikosi cha kwanza cha Ujerumani ili kucheza kwenye mchezo huo wa leo.
No comments:
Post a Comment