Kombe la Dunia; Kante na Giroud waanza vyema, na habari nyengine - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Kante na Giroud waanza vyema, na habari nyengine

Share This

Michezo miwili imeshakamilika mpaka sasa ambayo inawahusisha nyota wa kikosi cha Chelsea katika timu zao za taifa huko nchini Urusi kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

Ufaransa 2-1 Australia
Mchezo wa mapema kabisa ukiwahusisha nyota wawili wa Chelsea, N'Golo Kante aliyecheza dakika zote 90' za mchezo pamoja na mshambuliaji Olivier Giroud aliyeingia kama mchezaji wa akiba huku akija na neema ya kutoa pasi ya mwisho iliyoihakikishia timu yake ya Ufaransa mwanzo mzuri kwa kuondoka na ushindi huo wa magoli 2-1.

Argentina 1-1 Iceland
Willy Caballero kwa sasa ndiye kipa nambari moja kwenye kikosi cha Argentina na anakuwa golini wakati timu yake ikianza kwa kupata sare ya 1-1 dhidi ya timu ngumu ya Iceland.

Michezo uliosalia;
Nigeria vs Croatia
Mchezo uliosalia jioni ya leo ukiwahusisha nyota wa Chelsea ni pamoja na huu ambao unawahusisha Victor Moses pamoja na Kenneth Omeruo ambao wanatakiwa kupambana ili kujihakikishia ushindi na uongozi kwenye kundi lao.

Denmark vs Peru
Andreas Christensen ataiongoza tena timu yake ya taifa ya Denmark kupambana kwenye mchezo wao wa kwanza huku ikihitaji ushindi ili ijiweke kwenye nafasi nzuri ya kufudhu hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment