Chelsea yatengenewa dau nono kwa Kante - Darajani 1905

Chelsea yatengenewa dau nono kwa Kante

Share This

Klabu mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa, PSG wanatajwa kuanza taratibu za kumnasa kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante ambaye siku kadhaa nyuma iliripotiwa wameanza mazungumzo ya kumnasa.

Taarifa zilizopo zinadai kwamba klabu hiyo imeandaa kiasi cha paundi milioni 90 ili kuishawishi Chelsea kumnasa nyota huyo raia wa Ufaransa ambaye ni mchezaji bora wa Ufaransa anayecheza nje ya nchi hiyo.

PSG wanamtaka nyota huyo katika mbio zake za kutaka kupambania mafanikio nje ya Ufaransa na wanategemea kama wakimpata nyota huyo atatengeneza ukuta mzuri huku nyota wake Neymar na Mbappe wakisaidia kwenye mashambulizi.

No comments:

Post a Comment