Chelsea yaanza mazungumzo ya kumnasa nyota wa AS Roma - Darajani 1905

Chelsea yaanza mazungumzo ya kumnasa nyota wa AS Roma

Share This

Klabu ya Chelsea inatajwa kuanza mazungumzo ya kukamilisha usajili wa nyota raia wa Ugiriki anayeichezea klabu ya AS Roma ya nchini Italia, Kostas Manolas.

Manolas mwenye miaka 27 anatajwa kufukuziwa na Chelsea inayotajwa kuwa tayari kutoa paundi milioni 33 ili kumnasa nyota huyo anayefukuziwa pia na klabu ya Zenit St. Petersburg.

Chelsea inatajwa kuanza mazungumzo na wawakilishi wa nyota huyo anayecheza nafasi ya ulinzi ambapo ripoti hiyo imetolewa na mwandishi habari raia wa Italia.

No comments:

Post a Comment