Nyota wa kikosi cha Chelsea, Cesc Fabregas amekuwa ni moja ya raia wa Hispania aliyeachwa kwenye kikosi cha timu hiyo ya Hispania kinachoshiriki Kombe la Dunia linaloendelea huko nchini Urusi huku nyota mwenzake wa Chelsea, Cesar Azpilicueta akijumuishwa kama mchezaji pekee kutoka Chelsea.
Lakini hii haionyeshi kumfurahisha Fabregas ambaye amefanikiwa kuichezea timu hiyo ya Hispania zaidi ya michezo 100 huku akiwa mmoja ya wachezaji kwenye kikosi kilichoibuka mabingwa kwenye michuano ya Euro kwa mwaka 2008 na mwaka 2012 lakini pia kwenye kikosi kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2010.
Nyota huyo anayecheza kama kiungo anaamini kukosa kwake nafasi ya kuitwa kwenye kikosi kinachoshiriki Kombe la Dunia mwaka huu ni kutokana na kocha wa Chelsea, Antonio Conte kutompatia muda mwingi kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea kilichomaliza msimu kwa kushinda taji moja la Kombe la FA.
Fabregas aliongea maneno hayo alipokuwa kwenye mahojiano na chombo cha habari cha BBC akifanyiwa mahojiano na mtangazaji maarufu Gary Lineker na kuendelea kusema halaumu sana kwa kikosi kilichoteuliwa na kocha Lopetegui ambaye alitimuliwa kazi siku kadhaa kabla ya kuanza michuano hiyo kwa kuchaguliwa kuwa kocha wa Real Madrid wakati timu ya Hispania ikiwa inajiandaa.
No comments:
Post a Comment