CHELSEA BADO KUMWAGA MAPESA TU KWA LEMAR - Darajani 1905

CHELSEA BADO KUMWAGA MAPESA TU KWA LEMAR

Share This
Kocha wa klabu ya As Monaco, Leonardo Jardim ni kama ameonyesha taa ya kijani kwa mchezaji wake Thomas Lemar kuondoka klabuni hapo ambaye pia anatajwa kutakiwa kwa karibu na kocha wa Chelsea, Antonio Conte.

"Dirisha la usajili limefunguliwa, na kama unavyojua ikifikia kipindi iki mambo huwa yanakwenda ovyo ata kama klabu haipendi haswa kwa klabu ya Monaco, tunashindwa kusema hapana ata kama hatutaki kumuuza nyota wetu, ni kama ilivyokea kwa Liverpool walipomuuza Couinho. Natamani kuwa pamoja na Lemar hapa hata kama ikikaa kwa miaka 10 nataka naye awe pamoja nami lakini ni lazima nikiri ni ngumu kumbakisha" alisema kocha huyo.

Kwa kauli hiyo inamaanisha Chelsea inaweza kutupa nyavu na doano kwa nyota huyo ili kumnunua katika dirisha hili la usajili ukizingatia wao kama Monaco wamekiri wanaweza kumuachia nyota huyo japo wenyewe wanapenda aendelee kubaki. Kulikuwa na taarifa zinazodai kuwa kocha Antonio Conte anawataka nyota watatu ambao ni Thomas Lemar, Leon Bailey ambaye mwenyewe ni raia wa Jamaica na anaichezea klabu ya ligi kuu ya Bundesliga, Bayer Leverkusen pamoja na Ross Barkley ambaye tayari ashatua klabuni na kukabidhiwa jezi yenye namba 8.

No comments:

Post a Comment