VITA YA MOURINHO NA CONTE YAZIDI KUNOGA - Darajani 1905

VITA YA MOURINHO NA CONTE YAZIDI KUNOGA

Share This
Baada ya kipindi cha muda kidogo kuwa katika ugomvi wa maneno baina ya makocha wawili wa klabu tofauti yaani kocha wa Chelsea na Manyumbu sasa huenda ugomvi huo ukaamia sehemu nyengine kwa makocha wa klabu za Chelsea, Antonio Conte na kocha wa Manyumbu(Man utd), Jose Mourinho ambaye kabla alishawai kuifundisha Chelsea katika vipindi viwili tofauti.

Ugomvi huo sasa unatajwa kuamia kwenye kugombania nafasi ya ukocha wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa ambapo nafasi hiyo kwa inayoshikiliwa na kocha Unai Emery ambaye anatazamiwa kuiacha mwishoni mwa msimu huu na maboss wa klabu hiyo wanawataja makocha Conte na Mourinho kama mmojawao atachukua nafasi ya kocha huyo katika timu hiyo tajiri nchini Ufaransa.

Kocha Antonio Conte amekuwa akitajwa na magazeti na mitandao ya michezo barani Ulaya kwamba msimu huu huenda ukawa wa mwisho kwake kuwa klabuni Chelsea huku kocha Massimiliano Allegri akitajwa kukubali kuiacha Juventus na kutua Chelsea ili kurithi mikoba ya kocha muitaliano mwenzake.

No comments:

Post a Comment