Klabu ya Barcelona inayoshiriki ligi kuu Hispani maarufu kama La Liga imekubali kumwachia nyota wa klabu ya Gremio ya nchini Brazil, Arthur Henrique ajiunge na Chelsea mara baada ya kushindwana juu ya mahitaji ya klabu yake ambapo klabu hiyo ilikuwa tayari kumuachia nyota huyo kwa dau la paundi milioni 45.
Chelsea ilikuwa ikimfukuzia pia nyota huyo ingawa Barca ndio ilikuwa inapewa nafasi kubwa kumnasa kabla ya baadae kughairi ambapo sababu nyengine inayotajwa kuifanya Barca ighaili ni kutokana na kumpata nyota mwengine wa kibrazil, Phillipe Coutinho aliyesajiliwa kutokea Liverpunga(Liverpool).
Chelsea itatakiwa kuendeleza mpango wa kumnasa nyota huyo mwenye miaka 21 huku akiwa na sifa kubwa ya kuwa mmoja ya viungo bora nchini Brazil ambapo kwa kumpata huyo itaweza kupata kzazi kipya cha Chelsea kwa maana waliopo sasa wanaelekea kuchoka kutokana na umri mkubwa waliokuwa nao.

BARCA YAMWACHIA NYOTA WA BRAZIL ATUE CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment