UNAMTAKA BAILEY? UMESIKIA HII - Darajani 1905

UNAMTAKA BAILEY? UMESIKIA HII

Share This
Chelsea imekuwa ikitajwa kuhusishwa na nyota kadhaa katika dirisha hili dogo la usajili, lakini kati ya nyota waliokuwa wanatajwa kuwaniwa na Chelsea bsi ni yule kinda anayeichezea klabu ya Bayer Leverkusen inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga, Leon Bailey ambaye kwa sasa ana miaka 20, na kutimiza kwake miaka 21 ni mpaka ufike mwezi Agosti mwaka huu.

Raia huyo wa jamaica ambaye alishawai kuwa kwenye kikosi cha klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania, Mbwana Samatta anatajwa kuwa kwenye rada za kocha Antonio Conte, lakini kiongozi wa klabu yake umemsikia alichokisema.

Ana jeuri huyo, eti amesema hii "Sisi ndio klabu pekee ambayo kama klabu kama Bayern ikimtaka mchezaji kwetu tunaweza kusema Hapana, na kama unavyofahamu tumekuwa na wachezaji nyota wanaotakiwa na klabu kadhaa na mara zote tunauza pale tunapotaka. Kama nyota mwenyewe atataka kuondoka, tutakaa chini kwa pamoja na kuamua lipi lifanyike" alisema kiongozi huyo anayeitwa Rudi Voller akionyesha kutotatizwa wala kupata tabu kwa kuwa eti nyota wake anatakiwa na klabu kubwa kama Chelsea.

No comments:

Post a Comment