CHELSEA IANGALIE KWA MARCOS ALONSO KABLA YA KUMLETA SANDRO - Darajani 1905

CHELSEA IANGALIE KWA MARCOS ALONSO KABLA YA KUMLETA SANDRO

Share This
Chelsea imekuwa ikitajwa kumleta nyota wa klabu ya juventus, Alex Sandro ambaye thamani yake inatajwa kuwa paundi milioni 60, kiasi ambacho ni kikubwa kwa nyota huyo ukilinganisha anatazamiwa kuja Chelsea kumpa changamoto mlinzi wa kushoto, Marcos Alonso ambaye wanacheza nafasi moja katika mfumo wa kocha Antonio Conte ambapo anatumia mfumo wa 3-4-3 au ata 3-5-2.

Alex Sandro amekuwa akifukuziwa na Chelsea kwa karibu toka katika dirisha kubwa la usajili lililopita huku Chelsea ikipigwa chini na Juventus licha ya kujaribu kumsajili zaidi ya mara moja.

Embu tupitie wa vipeengele hivi tuone je ni kweli Chelsea inatakiwa kutumia kiasi chote hicho kwa nyota huyo wkati huenda Marcos Alonso akwa bora kuliko hata Sandro.

Kuhusika katika magoli
Ni beki mmoja tu aliyemzidi Marcos Alonso katika kuhusika kwenye magoli mengi msimu huu katika ligi bora tano barani Ulaya, ambaye ni Phillipe Max ambaye mwenyewe amehusika kwenye magoli 10 huku Marcos Alonso akihusika kwenye magoli 7(magoli 6 na pasi ya mwisho moja) huku akiwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Chelsea ukilinganisha na kumleta Alex sandro ambaye mwenyewe mpaka sasa amehusika kwenye magoli 4(goli moja na pasi za magoli 3), sasa je kuna haja ya kuachana na Marcos Alonso ambaye pia ameizoea ligi na kumleta huyo sandro ambaye atakuwa mgeni na kwa dau kubwa?

Ubora wa mchezaji binafsi
Sawa ndio kwa upande wa kukokota mpira Marcos Alonso amezidiwa ambapo Alex Sandro ana wastani wa 1.9 wakati Alonso ana 0.5 na hata kwenye pasi za muhimu Alonso napo amemwagwa akiwa na wastani wa 1 huku Sandro akiwa 1.2 lakini ukiangalia katika upande wa kuzuia Marcos amemzidi Alex Sandro maana Marcos ana wastani wa 1.4 wakati Sandro ana 0.9.

Ukiangalia kwa baadhi ya sababu hizo unaweza kuona kwa kiasi gani Chelsea haina haja ya kutumia kiasi kikubwa kama hicho ili kumsajili mtu ambaye kitu anachokuja kukifanya huenda kikawa kidogo kuliko kinachofanywa sasa na Marcos Alonso, lakini pia kumbuka ligi anayocheza Alex Sandro ya Serie A huko nchini Italia haina ugumu kama anayocheza Marcos Alonso kwa maana hiyo huenda Chelsea ikafanikiwa kumnasa Alex Sandro ila kutua kwake Chelsea kunaweza kukamfanya ashuke kisoka kutokana na ugumu wa ligi.

Lakini kama alivyosema Antonio Conte kuwa anamtaka mtu atakayeweza kumpa changamoto Marcos Alonso kutokana na nafasi hiyo kuwa peke yake pale Chelsea huku Kennedy akionekana kushindwa kumpiku Marcos basi ni vyema kikatumika kiasi kidogo kumsajili mtu atakayekuja kukaa hata benchi, maana ni ngumu kumleta Alex Sandro kwa dau kubwa kama hilo la paundi milioni 60 alafu akaja Chelsea kukaa benchi.

No comments:

Post a Comment