CHRISTENSEN ATISHIWA CHELSEA - Darajani 1905

CHRISTENSEN ATISHIWA CHELSEA

Share This
Nyota mpya wa klabu ya Chelsea, Andreas Christensen ambaye upya wake upo kwa vile ameanza kucheza timu ya wakubwa kayika msimu huu ambapo kabla alikuwa kwenye akademi ya Chelsea kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Borrusia Monchnglebach inayoshiriki ligi kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga amesigfu jinsi Chelsea ilivyo kwa sasa akiogopeshwa na ugumu wa kikosi hicho.

"Ukiwa hapa huwezi kukaa kwa raha, kutokana na kugoombania namba na nyota kadhaa unapcheza nao nafasi moja. Timu inawachezaji wengi na katika nafasi moja unakuta kuna wachezaji wengi wenye ubora na hivyo kukufanya unapopata nafasi kujitahidi kutofanya makosa. Ni jambo zuri maana napendezwa na hali kama hii maana klabu kubwa kama hii sio rahisi kwa mtu kupata nafasi na kama akipata basi anacheza kwa ubora ili asiweze kupoteza nafasi siku nyengine" alisema nyota huyo raia wa Denmark mwenye miaka 21 kwa sasa.

"Ni vyema kufanyiwa mabadiliko kila baada ya mchezo flani, lakini huwa unatamani ucheze kila mchezo na unapocheza mwisho wa mchezo unajihisi kuchoka lakini kwa kuwa unapenda soka haulalamiki" aliongezea nyota huyo ambaye aliisaidia timu yake ya taifa kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia mwaka huu uko nchini Urusi.

Ni vyema kuwa na kikosi kipana kama hivi, lakini haitakiwi mchezaji ukubali kushindwa na badala yake inatakiwa upambane zaidi, hongera Christensen na uendelee kupambana zaidi maana sisi mashabiki tunakutegemea sana

No comments:

Post a Comment