CONTE AKUTWA NA MAJANGA CHELSEA - Darajani 1905

CONTE AKUTWA NA MAJANGA CHELSEA

Share This
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte mchana wa leo amekutwa na majanga akiwa klabuni Chelsea kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo maarufu kama Cobham Stadium mara baada ya upepo mkali kutokea maeneo hayo na kuaribu gari la kocha huyo aina ya Nissan Juke lililokuwa limeegeshwa katika eneo la kuegesha magari.

Akihojiwa mtu mmoja klabuni hapo ambaye yeye alilishuhudia tukio ilo kwa kamera za siri, CCTV alisema "Steve Atkins alikuwa anaenda lilipo gari lake ambalo liliegeshwa kando na gari la Conte ndipo meza ndogo ya kioo iliyopeperushwa na upepo mkali ikadondokea kwenye gari la Conte huku Atkins akilikwepa na kudondokea pembeni kutokana na mtikisiko uliotokana na upepo huo" alisema mtu huyo.

Steve Atkins ambaye alikoswa na ajali hiyo na huku gari lake likinusurika kupatwa na kadhia hiyo ni kiongozi ambaye huwa anasimamia mikutano ya kocha Antonio Conte anapofanya na waandishi wa habari. Muhimu hakuna hasara kubwa iliyotokana na kadhia hiyo na hakuna hasara kubwa iliyotokea zaidi ya mali kadhaa.

Pole kocha Antonio Conte na uongozi wa Chelsea kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment