Jana katika jiji la London ulichezwa mchezo mkubwa wa Basketball ambapo klabu za Boston Celtics dhidi ya Philladephia 76ers zilikuwa uwanjani kupambana, lakini jambo kubwa kuihusu Chelsea ni pale Eden Hazard alipotoa kauli iliyokuwa gumzo kwenye magazetie mengi na hata mitandao.
"Usiondoke Chelsea"
"Haitotoke" alijibu Eden Hazard mara baada ya shabiki mmoja kupiga nae picha na kumwambia asiondoke klabuni Chelsea, lakini pia mara baada ya tukio hilo, chombo kimoja cha habari kilimuuliza kama atasaini mkataba mpya klabuni Chelsea ambapo mwenyewe alijibu "Ndiyo"
"Nitasaini mara baada ya Thibaut kufanya ivo" alisema Hazard.
Lakini pia jana kulikuwa na habari zilizoshika vichwa vya habari vingi mara baada ya redio ya Ufaransa, RMC kuripoti kuwa nyota huyo anajiandaa kutua Real Madrid katika kipindi cha kiangazi ambapo kutakuwa na dirisha kubwa la usajili.
Sasa sijui ni lipi la kulielewa maana kila siku inatoka ripoti mpya, ila cha muhimu tusubiri tuone lipi ni lipi!
No comments:
Post a Comment