POLISI WAINGILIA KATI USAJILI WA BARKLEY - Darajani 1905

POLISI WAINGILIA KATI USAJILI WA BARKLEY

Share This

Ijumaa iliyopita Chelsea ilikamilisha usajili wa nyota Ross Barkley kutoka Everton kwa dau la paundi milioni 15 na kumpatia mkataba wa miaka mitano na nusu, lakini baada ya usajili huo kiongozi wa serikali mwenye cheo cha umeya jijini Merseyside aliandika barua kwa polisi wa jiji hilo ili ufanyike uchunguzi katika biashara hiyo iliyofanyika kati ya Chelsea na Everton katika kuuziana nyota huyo mwenye miaka 24.

Meya huyo ametaka uchunguzi ufanyike mara baada ya kushangazwa na dau dogo ililolitoa Chelsea ili kumnasa mchezaji huyo wakati miezi sita kabla katika dirisha la usajili kubwa, Chelsea ilikuwa tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 35 kabla ya dili hilo kuvunjika kutokana na mchrzaji huyo kuwa majeruhi.

Lakini sasa ameshakaribia kupona kabisa inakuwaje Chelsea imnase kwa paundi milioni 15? hilo ndilo swali la meya huyo ambaye baadae akaandika barua kuipelekea polisi na hata chama cha soka Uingereza(FA) na pia akapeleka kwa Ligi kuu Uingereza ili usajili wa nyota huyo uchunguzwe.

Ila pia jana, mwenyekiti mtendaji au rais wa klabu ya Everton alipoulizwa kuhusu usajili huo alidai hana tatizo katika usajili huo maana mchezaji alishaamua kuondoka.

No comments:

Post a Comment