Mara baada ya nyota wa Chelsea, Alvaro Morata kupokea lawama nyingi kutokakwa mashabiki wa Chelsea haswa kulalamikiwa kwa kiwango butu alichokionyesha katika michezo miwili aliyocheza dhidi ya Arsenyani(Arsenal) ule wa ligi kuu Uingereza uliochezwa wiki iliyopita na huu wa jana ambao yote ametoka bila kufunga, mlinziwa Chelsea, Antonio Rudiger ambaye walisajiliwa wote kwa kipindi kimoja katika dirisha kubwa la usajili amekuwa upande wa Morata na kumtetea nyota mwenzake huyo.
"Kila mshambuliaji anapenda kufunga. Hii ya kupata nafasi na kushindwa inaweza kumtokea mtu yoyote, nadhani cha muhimu kwa Morata ni kufanya juhudi na kupambana zaidi haswa katika kipindi hichi kigumu kwake, naamini atarudi katika ubora aliokuwa nao mwanzo" alisema Rudiger ambaye naye alikuwepo jana na alicheza dakika zote za mchezo huo wa nusu fainali ya kombe la ligi.
"Sio mashabiki wanamtegemea tu, hata sisi kama timu tunamuangalia yeye lakini sio kumlaumu pale anaposhindwa kufuga naamini anatamani sana kufunga ila bahati haipo kwake kwa sasa" alisema Rudiger alipoulizwa nafasi ya Morata katika Chelsea ya sasa.
"ndiyo anaweza kufanya hivyo, kama alivyopata nafasi katika mchezo dhidi ya Bournemouth, alipata nafasi moja na akaitumia vyema kutupatia ushindi" alijibu alipoulizwa kama anadhani Morata ataweza kuifunga Arsenyani katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa tareh 24 ya mwezi huu kama ataweza kuipeleka Chelsea katika fainali ya kombe la ligi.

RUDIGER AMTETEA MORATA KWA KIWANGO BUTU
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment