HAZARD NJIANI KUTUA REAL MADRID - Darajani 1905

HAZARD NJIANI KUTUA REAL MADRID

Share This
Baada ya mfululizo wa fununu na tetesi nyingi juu ya nyota wa Chelsea, Eden Hazard kutakiwa na klabu ya Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Hispania maarufu kama La Liga na taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya maarufu kama Uefa Champions League. Chomo cha habari cha RMC ambayo ni redio ya nchini Ufaransa kimeeleza kuwa nyota huyo atajiunga na klabu hiyo katika dirisha kubwa la usajili ambalo litakuwa kipindi cha kiangazi.

Chombo hicho kinadai kocha wa klabu hiyo, Zinedine Zidane ndiye anamuwania kwa karibu nyota Hazard lakini pia kukiwepo na taarifa kuwa Hazard anatamani kucheza chini ya kocha huyo kutokana na kuvutiwa kwake na kocha huyo pindi alipokuwa mchezaji.

Zinedine Zidane alikuwa nyota wa klabu kadhaa kama Juventus na Real Madrid na katika kipindi hicho alikuwa akicheza katika ubora wa hali ya juu na hivyo kuwa mmoja wa wachezaji vipenzi wa Eden Hazard na sababu hiyo inatajwa kumfanya Hazard atamani kuwa chini ya kocha huyo na huku kukiwa na taarifa kuwa Hazard aligoma kusaini mkataba mpya mara mbili klabuni Chelsea ili aangalie uwezekano wa kuungana na kocha huyo,

No comments:

Post a Comment