Chombo cha habari za michezo Sky Sports kimeandika makala kumuelezea nyota wa Chelsea, kinda mwenye nywele nyingi Ethan Ampadu huku wakifika mpaka nyumbani au mtaani alipozaliwa huku Chelsea ikimsajili mwaka 2017 akitokea klabuni Exeter ambapo hapo alianza kucheza soka lake katika akademi hiyo.
Nyota huyo ambaye ni raia wa Wales mwenye miaka 17 kwa sasa aling'aa katika mchezo wa robo fainali ambapo Chelsea ilimenyana dhidi ya Bournemouth, na katika mchezo huo aliibuka nyota wa mchezo huku akionyesha kiwango cha hali ya juu katika nafasi ya ulinzi wa kati huku wengi wakimuona kama mrithi sahihi wa David Luiz klabuni hapo huku akifanya makubwa katika mchezo ambapo moja ya jamb kubwa alilowashangaza wengi ni utulivu wake na uwezo mkubwa wa kutoa pasi, katika mchezo huo alitoa pasi 87 ambazo zilizofika kati ya 88, yani alipoteza pasi moja tu.
Lakini kabla ya mchezo huo, alicheza mchezo wake wa kwanza klabuni Chelsea akiingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Huddersfield ambao ulikuwa ni mchezo wa ligi kuu huku pia akiichezea timu ya taifa ya Wales katika mchezo dhidi ya Ufaransa na hata Panama.
Klabuni alipoanzia soka(Exeter city);
"Hakukuwa na wachezaji wengi waliojiunga na Exeter ya vijana chini ya miaka 7 ambao wao ilitakiwa wacheze mpaka watakapopandishwa na kuingia chini ya miaka 9 kwa hiyo hatukutenga kuwa na wachezaji wa chini ya miaka 7, ni Ethan tu aliyefika akiwa na miaka 7 na kuomba ajiunge na timu, ilitubidi tumkubalie lakini tulimpa nafasi ya kucheza na wenzake wenye miaka 9, " Hayward aliiambia Sky Sports. "Licha ya kuzidiwa miaka miwili ila alionyesha kipaji cha hali ya juu na ukomavu mkubwa"
"Hakukuwa na wachezaji wengi waliojiunga na Exeter ya vijana chini ya miaka 7 ambao wao ilitakiwa wacheze mpaka watakapopandishwa na kuingia chini ya miaka 9 kwa hiyo hatukutenga kuwa na wachezaji wa chini ya miaka 7, ni Ethan tu aliyefika akiwa na miaka 7 na kuomba ajiunge na timu, ilitubidi tumkubalie lakini tulimpa nafasi ya kucheza na wenzake wenye miaka 9, " Hayward aliiambia Sky Sports. "Licha ya kuzidiwa miaka miwili ila alionyesha kipaji cha hali ya juu na ukomavu mkubwa"
"Ulipofika mwisho wa mwaka, ile timu ya miaka 9 ilitakiwa ipande na kuingia kwenye chini ya miaka 10, lakini nilipokuwa na Ethan(Ampadu) na baba yake tukiangalia maendeleo yake ya mwaka mzima ambao ndio ulikuwa mwaka wake wa kwanza kuwa hapa, Ethan alichagua kucheza tena kwenye timu ya chini ya miaka 9 kwa mwaka mwengine, lakini kutokana na umri wake ingawa tulikubali ila tulikuwa nae karibu sana"
Baba wa Ethan, Kwame Ampadu alicheza soka katika klabu ya wakubwa ya Exeter kwa maana hiyo ilikuwa rahisi kwake kuungana na mwanae pale alipokuwa akifanya mazoezi na vijana wa akademi wa timu hiyo ambapo Ampadu alikuwa mmojawao.
Na jambo la kushangaza kwa Ampadu alikuwa na uwezo mkubwa mpaka kufikia kucheza timu ya vijana ya chini ya miaka 18 huku mwenyewe akiwa na miaka 13.
"Ilikuwa ni mara ya kwanza kutokea klabuni hapa kwa mchezaji kucheza kwenye timu iliyomzidi miaka mitano. Muda mwengine alikuwa anapata tabu kucheza nao kutokana na tofauti ya umri, ila haikuwa tatizo sana maana pia alikuwa akifanya vizuri. Wakati mwengine alikuwa akiungana na wenzake wenye umri sawa na hivyo ilikuwa ikimsaidia kupata changamoto kutoka huku na huku" alisema Haywkard.
"Kuna kipindi klabu ilihitaji wachezaji wanaocheza nafasi tano tofauti, jambo la kushangaza Ethan alikuwa na uwezo wa kucheza nafasi nne kati ya hizo zilizotakiwa maana sifa yake kubwa alikuwa mpambanaji na alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza soka kwa miguu yote." alisema Haywkard.
Katika sehemu ya pili nitakuletea mahojiano yaliyofanyika kati ya Sky Sports na nahodha wa zamani wa Tottenham, Steve Perryman ambaye naye alihusika katika kumchunga Ethan Ampadu mpaka kufikia hapa alipo. Tukutane sehemu ya pili...
No comments:
Post a Comment