Bodi ya klabu ya Chelsea ikiongozwa na mwenyekiti au rais wa klabu hiyo, Bruce Buck leo imekamilisha usajili mpya katika bodi ya klabu hiyo mara baadaya kumsainisha mtendaji mpya aliyechukua nafasi ya mtendaji wa zamani, Michael Emenalo ambaye kwa sasa anafanya kazi klabuni AS Monaco, na toka kuondoka kwake nafasi hiyo haikupata mrithi mpaka hii leo ambapo rais wa Chelsea amemtangaza ndugu Guy Laurence kuwa ndiye atakuwa mrithi wa Emenalo.
Guy Laurance alizaliwa mwaka 1961 jijini Manchester nchini Uinngereza kwa sasa akiwa na familia yenye watoto watatu lakini kabla ya kuteuliwa na Chelsea ambapo uteuzi huo umefanyika leo alishawai kufanya kazi katika kampuni ya Vodafone UK lakini pia akiwa mmiliki halali wa kampuni ya mawasiliano ya Rodgers Communication iliyopo nchini Uingereza.
Lakini pia katika michezo ameshafanya kazi katika kampuni inayomiliki baadhi za klabu nchini Marekani ya Maple Leaf Sports and Entertainment. Majukumu yake kwenye klabu atakuwa na nafasi ya kujaribu kuongeza kipato cha klabu kwa kutafuta mapato na kujiwekeza zaidi.
Karibu Darajani

BODI YA CHELSEA YAFANYA USAJILI MPYA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment