CONTE NJE? - Darajani 1905
Kumekuwa na taarifa zilizozagaa sana mtandaoni na haswa kwenye magazeti kukiripotiwa kumhusu kocha wa Chelsea, Antonio Conte kuwa mrithi wake ashapatikana na huenda kocha huyo akaachana na Chelsea mara baada ya msimu huu kuisha.
Habari hizo zimeanza kuripotiwa na gazeti la nchini kwao Italia maarufu kama Carriero dello Sporte likimwelezea kocha Antonio Conte kuachana na Chelsea mwishoni mwa msimu huu huku kocha mwenzake muitaliano, Massimiliano Allegri ndiye anayetajwa kuchukua nafasi yake klabuni Chelsea.

Mwezi Oktoba mwaka 2017, kocha Antonio Conte aliwai kuulizwa kuhusu tetesi zake zinazomhusisha kuondoka klabuni hapo, na alijibu akisema "Kuna tetesi mbaya ambazo zimekuwa zikijaribu kutufanya mimi, klabu na wachezaji wangu tuingie kwenye mgogoro lakini pia nawaruhusu muweze kuandika kama klabu inataka kunifukuza na hata kuandika kuhusu mgogoro wangu pamoja na wachezaji wangu. Ila nahitaji kuheshimiwa katika hili" alijibu maneno hayo akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari akikana kuondoka klabuni hapo.

Lakini Darajani 1905 inaelewa sababu kubwa inayomfanya kocha Antonio Conte ni kupoteza mvuto kwa baadhi ya wachezaji kutokana na kocha huyo kuingia kwenye migogoro na baadhi ya wachezaji ambao walikuwa vipenzi kwa wachezaji wengine na hata kwa baadhi ya mashabiki ingawa kuna baadhi ya takwimu ziliwai kufanywa na kuonekana kocha huyo bado ana mvuto kwa mashabiki na hata kwa wachezaji.

Kuondoka kwa Diego Costa tena kwa mgogoro mkubwa huku nyota huo akigoma kabisa kurudi Chelsea baada ya kuripoti alitumiwa ujumbe na kocha Conte kuwa hayupo kwenye mipango tena ya Chelsea na tena kuripotiwa kuwa na mgogoro na mlinzi David Luiz kunaweza kuwa sababu ya kocha huyo kupunguza mvuto na timu ukizingatia nyota hao mara zote walikuwa burudani na furaha kwa wachezaji na hata mashabiki.

No comments:

Post a Comment