Nyota mpya wa Chelsea, Ross Barkley ambaye uhamisho wake wa kuja Chelsea ulikamilika ijumaa iliyopita akitua Chelsea kwa dau la paundi milioni 15, dau ambalo limezua mzozo mkubwa klabuni alipotoka, Everton (kusoma mzozo uliotokea, Bonyeza Hapa) akisaini kuichezea Chelsea kwa miaka mitano na nusu huenda akawepo katika mchezo wa jumamosi huu ambapo Chelsea itashuka uwanjani Stamford Bridge kumenyana na Leicester city katika mchezo wa ligi kuu.
Nyota huyo alitambulishwa rasmi kwa mashabiki hapo jana wakati mapumziko katika mchezo wa Chelsea ilipomenyana dhidi ya Arsenyani (Arsenal) na mchezo huo kuisha kwa sare ya 0-0.
Chelsea itashuka katika mchezo huo ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu huku kukitegemewa nyota huyo ambaye mpaka sasa hajacheza mchezo wowote katika msimu huu kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo akitegemewa kuwepo katika mchezo huo ambao kama Chelsea itapata ala tatu basi itapanda mpaka nafasi ya pili.
Ross Barkley alianza mazoezi yake binafsi ambapo alianza na mazoezi ya kumiliki mpira na hata mazoezi mengine mepesi siku kadhaa baada ya kusajiliwa huku ikitegemewa kuwai kurejea uwanjani ambapo hata kocha Antonio Conte alikiri kuwa nyota huyo alishaanza kufanya mazoezi ya pamoja na nyota wenzake na huenda akawepo katika mchezo wa hivi karibuni.

BARKLEY ATAMBULISHWA RASMI, KUWEPO DHIDI YA LEICESTER
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment