Mara baada ya Chelsea kumsajili nyota wa Ross Barkley aliyekuwa anaichezea klabu ya Everton akiwa amesajiliwa kwa dau la paundi milioni 15 huku pia akisaini mkataba wa miaka mitano na nusu kuichezea klabu hiyo, huko alipotoka maeacha moto ambao haijulikani utazimika lini.
Nyota huyo mara baada ya kusajiliwa na Chelsea, kulizuka mzozo mkubwa juu ya ada iliyotumika kumsajili nyota huyo aliyedumu mklabuni Everton kwa miaka 10 ambapo ilionekana dau lililotolewa na Chelsea lapaundi milioni 15 lilikuwa ni dogo kulingana na dau lililotolewa mara ya kwanza katika dirisha kubwa la usajili la mwezi Agosti mwaka jana ambapo Chelsea ilikuwa inakaribia kumnasa nyota huyo kwa kiasi cha paundi milioni 35 lakini amekuja kusajiliwa kwa kiasi kidogo sana kulinganisha ni lile dau la mwanzo ambapo usajili ulishindikana kutokana na Barkley kuwa na majeruhi.
Aliyeanza kulalamika alikuwa kiongozi wa serikali inapotokea klabu hiyo ya Everton ambapo alishangazwa kwa usajili huo kukamilika kwa dau dogo na kusema ataomba vyombo maalumu vifanye uchunguzi juu ya usajili huo akihisi huenda Chelsea imefanya udanganyifu, lakini leo imetoka taarifa kuwa kumbe dau ililotoa Chelsea ili kumsajili nyota huyo raia wa Uingereza, nusu yake alichukua wakala wa nyota huyo ambapo kiasi cha paundi milioni 7 kinatajwa kuchukuliwa na wakala na paundi milioni 8 ilichukuliwa na klabu.
Lakini kuna jengine tena likaibuka, mmiliki wa klabu ya Everton, Bill Kenwright naye ametoka huko alipo na kutoa neno juu ya mzozo huo akisema halaumu kama kuna udanganyifu umefanyika maana tatizo lilikuwa kwa mchezaji mwenyewe kuwa hakuwa tayari kuendelea kubaki na badala yake anataka kwenda kutafuta changamoto mpya kutokea sehemu nyengine.
Sasa je kwa kauli hii ya mmiliki huyo itazima cheche na moto unaowaka juu ya nyota huyu? Au ndio kesi hii itafika mbali namwishowe chama cha soka Uingereza, FA kuingilia?

BARKLEY KUTUA CHELSEA, KWAACHA MOTO EVERTON
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment