MAMBO 5 KUELEKEA CHELSEA vs ARSENAL - Darajani 1905

MAMBO 5 KUELEKEA CHELSEA vs ARSENAL

Share This
Hapa nimekuletea mambo matano unayopaswa kuyajua kuelekea mchezo wa kombe la ligi maarufu kama Carabao Cup utakaochezwa leo usiku pale Stamford Bridge ambapo Chelsea itaikaribisha Arsenyani(Arsenal) katika mchezo huo wa kwanza ambapo mchezo wa pili utachezwa tarehe 24-Januari ambapo mshindi wa jumla hapo ndio atacheza fainali ya kombe hilo ambapo atakutana na mmojawapo kati ya Mama site(Man city) au Bristol city.

1. Chelsea imeshinda michezo minne kati ya mitano iliyocheza dhidi ya Arsenyani katika michuano hii ya kombe la ligi mojawapo pale ilipoifunga katika nusu fainali na kwenda kushinda fainali nakuwa bingwa msimu wa 1997-1998 wakati kwa upande wa Arsenyani, wameshinda mara moja kati ya mara tano ilizokutana na Chelsea ambapo kushinda huko ilikuwa katika raundi ya nne hiyo ilikuwa msimu wa 1976-1977.

2. Chelsea haijapoteza mchezo wowote ilipocheza na Arsenyani nyumbani, yaani Stamford Bridge katika michuano yote ambapo wamekutana na klabu hiyo mara nane lakini Chelsea imeshinda mara 7 na kutoa suluhu mchezo mmoja.

3. Katika nusu fainali zote ambazo Chelsea imecheza katika michuano hii imefanikiwa kuvuka kucheza fainali mara nne (2005, 2007, 2008 na 2013) na imeshinda kufuzu mara moja tu kucheza fainali ambapo kipindi icho ilikuwa chini ya kocha Rafa Benitez, mwaka 2013 ilipotolewa na Swansea.

4. Arsenyani wanashiriki mara ya 15, ndiyo timu iliyoshiriki nusu fainali ya kombe hili la ligi mara nyingi ikiachwa na Liverpunga(Liverpool) tu ambayo yenyewe imeshiriki mara 17. Lakini Arsenyani pia ndio klabu iliyotolewa mara nyingi katika hatua hii ya nusu fainali, mara 7.

5. Msimu huu, Chelsea imeruhusu kufungwa goli kila inapofika dakika ya 90 katika michezo yake mitatu iliyopita.

No comments:

Post a Comment