NI VITA YA CONTE DHIDI YA WENGER - Darajani 1905

NI VITA YA CONTE DHIDI YA WENGER

Share This
Kuelekea mchezo wa leo usiku ambao utachezwa saa 5 usiku huku Chelsea ikiikaribisha klabu ya Arsenyani(Arsenal) katika mchezo wa hatu ya nusu fainali ya kombe la Carabao, makocha wa pande zote mbili yaani Antonio Conte wa Chelsea na Arsene Wenger kwa upande wa Arsenyani wametoa maneno yao ya mwisho kuelekea mchezo huo.

Kwa upande wa kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema "Unapocheza kila baada ya siku tatu ni muhimu uwe unabadilisha kikosi lakini muda huohuo timu yako inatakiwa iwe bora, nje ya hapo utajikuta unatupwa nje katika michuano. (vs Arsenyani) Ni mchezo mzuri kwetu, na wa muhimu maana ni nusu fainali na kama ukishinda unakuwa na nafasi ya kushinda taji. Tulistahili kufikia hapa tulipo na utakuwa mchezo mgumu kucheza dhidi ya Arsenal"

Lakini kwa upande wa Wenger, alisema "Tupo katika hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi na tuna nafasi ya kushina taji hili"

Je karata yako unaiweka wapi? Unadhani nani ataibuka mshindi katika mchezo huu?

No comments:

Post a Comment