Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amekuwa akitajwa kwa karibu kumtaka nyota wa klabu ya Bayern Munich ambaye ni raia wa Chile, Artulo Vidal na hata kuibuka taarifa kuwa wawili hao wanawasiliana kwa simu na hata kuwepo taarifa kuwa Chelsea imeshakbaliana na Artulo Vidal mwenyewe na hata kumtengea fungu la paundi milioni 13 kwa mwaka ambao ni kama mshahara, na ikaelezwa kuwa ni Bayern Munich tu wamebaki kumalizana na Chelsea ili kumuuza mchezaji huyo.
Lakini baadae kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes kutoa taarifa kuwa hakuna mawasiliano yoyote kati ya klabu yake na Chelsea na hata kusema kipindi hiki hakuna mchezaji yoyote anayeuzwa kutoka klabuni hapo. Mlolongo wote huo na matukio yote hayo lakini kiungo au muhusikamwenyewe hakuwai kutoa neno juu ya tetesi hizo, lakini leo ameibuka na akaongelea kuhusu tetesi hizo za yeye kutakiwa na Chelsea mambayo ipo chini ya kocha Antonio Conte ambaye walishawai kuwa wote klabuni Juventus kabla ya Vidal kuungana na Bayern na Conte kwenda timu ya taifa Italia na sasa Chelsea.
"Nimesikia tetesi hizo lakini nina malengo ya kuendelea kuwepo Bayern na nna furaha kuendelea kuwa mahali hapa. Sisi ni timu kubwa na tuna malengo makubwa, tunataka kushinda kila taji na hiyoo ndio nachokitaka kutoka hapa" alisema Vidal akieleza nia yake ya kutotaka kondoka Bayern.

VIDAL ATOA NENO KUTAKIWA NA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment