Chelsea yaingia kwenye uchunguzi na vyombo vinavyopinga maswala ya kibaguzi kwenye soka.
Baadhi ya mashabiki inaosadikika ni mashabiki wa Chelsea wameonekana kwenye video ikiwaonyesha mashabiki hao wakipiga saluti maarufu kama saluti ya NAZI uku wakiimba nyimbo za chuki kwa klabu ya Tottenham kwenye mchezo wa UEFA kati ya Chelsea dhidi ya Lille, mchezo uliochezwa 2-Oktoba.
Chelsea imeandika ripoti ikisema haina uhakika kwamba mashabiki hao walikuwa mashabiki wa Chelsea lakini itahakikisha inatoa ushirikiano wote utakaohitajika kwenye uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Chelsea imekuwa ikiongoza kuhusu kupinga vitendo vya kibaguzi uku Roman Abramovich akiongoza kwenye kusaidia kampeni hizo kupingwa.
Klabu ya Tottenham inatajwa ni klabu yenye upinzani sana na Chelsea haswa kwa upande wa mashabiki.
Labda utakuwa unajiuliza saluti ya NAZI inahusiana vipi na mashabiki wa Tottenham?
Ipo hivi, inasadikika mashabiki wengi wa Tottenham wana asili ya uyahudi kutoka nchini Israel, taifa ambalo lilifanyiwa ukatili mkubwa na manyanyaso mengi na nchi ya Ujerumani kipindi cha utawala wa dikteta, Adolf Hitler ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama cha NAZI.
Hivyo mashabiki hao wa Chelsea wamekuwa wakitumia historia hiyo ya asili ya mashabiki wa Tottenham kama shutma kwa dhihaka kwa mashabiki hao.
No comments:
Post a Comment