Chelsea yapata vikwazo kuhusu Stamford Bridge mpya - Darajani 1905

Chelsea yapata vikwazo kuhusu Stamford Bridge mpya

Share This
Mpango uliokuwepo wa Chelsea kuupanua uwanja wake wasasa unaochukua mashabiki 41,000 na kufanyiwa upanuzi na kuchukua mashabiki 60,000 ni kama unaenda kufa mara baada ya mpango huo kusimamishwa mwezi May mwaka 2018.


Inaelezwa kwamba serikali ya jijini London ilitoa kibali cha kuanza matengenezo ya uwanja uku tarehe ya mwisho ikiwa mwezi 31-March mwaka huu lakini mpaka sasa hakuna matengenezo wala dalili ya matengenezo kuwepo.


Moja kati ya vyanzo vya taarifa vinadai kwamba Chelsea haijali kuhusu kibali hicho kuisha muda wake maana wanaamini kufatilia kwa mara ya pili hakutokuwa na ugumu kama kufatilia mara ya kwanza.

Mpango huo uliopata kibali mwaka 2017, kibali kikiwekwa na meya wa jiji la London, Sadiq Khan ulisimamishwa uku moja kati ya sababu ambayo haikuwekwa wazi ni tajiri Roman Abramovich kumaliza kibali chake cha kuishi nchini Uingereza ingawa sababu hiyo haikuwekwa wazi na ripoti ya klabu kuhusu kusimama kwa mpango huo uliotarajiwa kuwa na bajeti ya paundi bilioni 1.

No comments:

Post a Comment