Kuna taarifa kadhaa zinawataja wawili hao kukaribia kuungana tena kwa mara ya tatu uku moja kati vyanzo mbalimbali vikimtaja nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo kuhusika pia kumleta muitaliano huyo mwenye asili ya Brazil kuungana na kocha wa klabu hiyo ya vibibi vya Turin.
Wawili hao wamefanya kazi pamoja klabuni Napoli kabla ya wote kutua Chelsea na mwaka jana Maurizio Sarri akaachana na Chelsea na kutua Juventus uku akimwacha Jorginho akiendeleza maisha yake ndani ya Chelsea.
Kuna taarifa kwamba Cristiano Ronaldo ambaye ni nyota wa Juventus anataka kuishawishi klabu hiyo ihakikishe inamsajili Jorginho kutoka Chelsea kwa kuwa anautambua sana mfumo wa Maurizio Sarri lakini pia kwasababu anaona nyota wa klabu yao, Miralem Pjanic ameonyesha kutotimiza majukumu sawia kama alivyokuwa akitimiza Jorginho.
Wakala wa Jorginho alipoulizwa kuhusu tetesi za Jorginho kutakiwa na Juventus alisema "Bila shaka timu nyingi zitaleta ofa ya kumtaka Jorginho, haswa kutokana na ubora wake na kwa nafasi anayocheza na majukumu anayotimiza kwa kipindi cha sasa ni wachezaji wachache wanaweza kutimiza majukumu yake."
"Ata Juventus wanaweza kuleta ofa ya kumsajili. Hakuna lisilowezekana, tusubiri tuone lakini tutahitaji kukaa chini na Chelsea tujadili kuhusu hili."
No comments:
Post a Comment