Nadhani utakuwa unamkumbuka yule kocha kijana zaidi aliyewai kupita klabuni Chelsea ingawa hakudumu klabuni hapo kwa muda mrefu ambapo alifika Chelsea mwaka 2011 na kufukuzwa mwaka 2012 kutokana na Chelsea kuwa na matokeo mabovu, wengi walikuwa wakimfahamu kama AVB ila jina lake kiurefu ni Andre Villas Boas ambaye baada ya kutimuliwa Chelsea akatimkia Tottenham sasa kocha huyo amepata ajali huko nchini Peru alipokuwa katikamashindano ya magoli ambapo ameingia huko akiwa kama mshiriki rasmi mara baada ya kuachana na soka.
Andre Villas Boas alipata ajali hiyo katika mashindano ya Dakar Rally ambapo ndio ilikuwa mara ya kwanza kwake kushiriki mara baada ya kuachana na majukumu ya soka ambapo alikuwa akiitumikia klabu ya Shanghai SIPG ya nchini China na kuamua kuingia katikamashindano hayo ya magari ambapo mara nyingi huwa yanafanyika jangwani.
Mara baada ya kupata ajali hiyo alikimbizwa haraka hospitalini na kuendelea na matibabu huku ikielezwa alipata majeraha ya mgongo.
Andre Villas Boas ndiye aliiachia Chelsea kwa kocha Roberto Di Matteo kwa kuchaguliwa kuwa kocha wa muda na kocha huyo kuisaidia Chelsea kutwaa taji lake la kwanza la klabu bingwa ya Ulaya.

KOCHA CHELSEA AACHANA NA SOKA, APATA AJALI MBAYA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment